Friday, November 18, 2016

PICHA 10: Muonekano wa ndani wa Ndege ya Donald Trump

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump anazidi kuzimiliki headlines kubwa wakati ikijiaandaa kuingia Ikulu ya White House. Mbali na nafasi aliyoipata mfanyabiashara huyo tajiri, tunafahamu kuwa Trump anamiliki ndege yake binafsi ambayo ndiyo anayoitumia kwenye safari zake kama usafiri wake binafsi.
Ndege hiyo aina ya Boeing 757  imetajwa kuwa na thamani ya £63m ambazo ni zaidi ya shilingi billioni 147 za kitanzania, ina uwezo wa kubeba abiria 239, ndani yake kuna Sinki la kunawia ambalo limetengenezwa kwa Gold pia seat zake ni sofa zenye urembo wa Gold.










Thursday, November 26, 2015

DEGREE ZAZIDI KUMIMINIKA KATIKA FAMILIA YA MZEE MUSSA

Tarehe 27 mwezi wa 11 mwaka 2015 mtoto wa kumi kati ya 11 katika familia ya mzee mussa ,Ally Mussa ataungana na wenzake katika siku ya mahafali ya 6 ya chuo kikuu cha dodoma ambapo anahitimu shahada ya awali ya elimu na sanaa,Bachelor of Art with education
Aidha tar 5 mwezi wa kumi na mbili mtoto wa tisa nae jina Mustafa Mussa atavaa joho kuhitimisha kutafuta degree ya awali ya sanaa na elimu, Bachelor of Art with education.

hii ni baada ya kutanguliwa na ndugu zao waliohitimu miaka ya nyuma na juzi tu mmoja ambae ni Zubeda Mussa yeyey alimaliza Phd kabisaaaa katika chuo cha laperanta nchini Finland

karibuni tuungane nakusheherekea sote.

MUSTAFA MUSSA
MALENGA WA KIZIGUA